Mfalme wa miduara nchini Tanzania, AT amemchana msanii Rama dee kwa kumwambia anapaswa awaheshimu watu waliomtangulia.

Hayo yamekuja siku chache baada ya msanii Rama Dee kusema kiwango cha ‘director’ Mkongwe Adam Juma kiko chini ya viwango katika kutayarisha na kutengeneza ‘video’ na kwamba anamtaka ajifunze kutoka kwa Hanscana.

Siku za nyuma Jambo hilo lilipelekea Adam kunukuliwa akisema Mimi nimepumzika na sitaki kufuatilia mambo hayo ya muziki kila mtu ana misimamo yake na kwa sasa nataka niache kabisa mambo ya muziki nataka nifanye mambo yangu mengine ni ‘relax’ na kama kuna mtu anahisi mimi ni mjinga au mpumbavu ‘it’s fine.

AT amesema wasanii ndiyo wanaongoza kwa kutokuwa na heshima, hivyo amewataka wasanii wenzake kuwa na heshima kwa watu waliowazidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *