Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amesema kuwa uwepo wa familia nyuma yake kunampa hasira ya kufanya muziki mzuri.

Aslay amesema kuwa wasanii wote ambao wanafanya muziki kutokana na sababu fulani nyuma yao kama hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kufika mbali.

“Kwanza kabisa sipendi msanii ambaye anavimba, napenda msanii anayefanya kazi kwa kuonyesha mimi nyuma nina watu/familia, kwa watu kama hao huwa nawaheshimu sana kwa sababu huwa na hasira na maisha halafu ukiangalia kazi zao lazima ziwe nzuri mmoja wapo ni mimi”.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa anajitahidi kufanya muziki kwa sababu kuna familia inamtazama na licha kujitahidi ana kipaji pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *