Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata askari ‘feki’ wa Jeshi la Magereza, B. 6034 CPL. Elia @SGT. Frank (28) akiwa amevaa sare za jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa mtuhumiwa huyo Elias Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Desemba mwaka jana.

Amesema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa na cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti na alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.

Kamishna Sirro amesema jadala lake litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi ingawa alimtaka kuomba radhi jamii.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi, Msingwa ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema: “Bahati mbaya siku ya jana (juzi) sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya kutoka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *