Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghan, Asamoah Gyan pamoja na wachezaji wengine zaidi ya 40 wanaocheza ligi ya Urabuni wameamriwa kunyoa nywele zao baada ya kuweka mitimdo ya ‘panki’ ambayo haikubaliki nchini humo.

 Kwa mujibu wa kanuni za muongozo za chama cha soka cha Falme za Kirabu ‘United Arab Emirates Football Association’ unyoaji wa panki ni marufuku michezoni.

Mshambuliaji huyo anachezea kwa mkopo timu ya Ali Ahli ya Falme za Kiarabu akitokea timu ya China ya Shanghai SIPG.

Mwaka 2012, golikipa wa timu ya Saudi Arabia, Waleed Abdullah alizuiwa kucheza mechi wakati timu yake ya Al Shabab kwa kunyoa ‘kinyume na maadili’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *