Klabu ya Arsenal imetambulisha ndege mpya ambayo itakuwa inaitumia kusafiria kwenda kwenye mechi zake za ugenini za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Ndege hiyo aina ya Emarates Airbus A380 ni ya kifahari na ina kila kitu kinachohitajika ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo im­epambwa na picha za mastaa watano wa timu hiyo; Hector Bellerin, Olivier Giroud, Santi Cazorla, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Ndege hiyo ikionekana kwa ndani
Ndege hiyo ikionekana kwa ndani

Kila mchezaji ana kitanda chake pamoja na chaneli za televisheni 2,500 na kila mchezaji ana TV yake.

Pia kuna baa ya kisasa yenye vinywaji vya kila aina, vyoo na mabafu lakini pia maz­ingira mazuri ya kukaa.

Klabu hiyo wataanza kuitumia ndege hiyo kwa mara ya kwan­za watakaposafiri kuifuata Bayern Munich mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *