Klabu ya Arsenal imekataa dau ya paundi milioni 50 kutoka kwa Manchester City kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez.

Sanchez alifungia Arsenal mabao 24 kwenye ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita lakini mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Arsenal wamekataa majaribio yoyote ya kutaka kumchukua Sanchez kufikia sasa na wangefurahia sana iwapo Raheem Sterling atakuwa kwenye sehemu ya mkataba wake kuhamia City.

Meneja wa City Pep Guardiola inadaiwa hata hivto kwamba anataka kumnunua Sanchez, 28, moja kwa moja.

Hata hivyo, hatua ya kumnunua inaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City.

Sterling, 22, anayechezea timu ya taifa ya England amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu.

Lakini hatahakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco.

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyopigwa 4-0 na Liverpool Jumapili iliyopita.

Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.

Mapema mwezi huu meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Sanchez anataheshimu uamuzi wake wa kutaka kusalia naye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *