Klabu ya Arsenal jana imefanikuwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuwafunga Middlesbrough 2-1 kwenye mechi iliyofanyika uwanja wa Riverside.

Mchezo huo ulianza polepole huku kila timu ikiangalia mwanya mpaka dakika chache kabla ya mapumziko free-kick ya Alexis Sanchez ilipowanyanyua kwenye viti mashabiki wa Arsenal.

Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Sanchez.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Sanchez.

Middlesbrough wakalipiza kisasi mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili pale ambapo Alvaro Negredo alipoitupia ndani krosi ya Sterwart Downing.

Hata hivyo Arsenal ilikuwa inazihitaji sana pointi tatu kwa hivyo Mesut Ozil akaokoa jahazi kwa kutupia lingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *