Arsenal wamalizana na Aubameyanga kutoka Dortmund

0
195

Klabu ya Arsenal imekamisha usajili wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre Aubameyang kutoka Borrussia Dortmund.

The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette.

Dortmund ilikuwa imesema kuwa itamuuza mcheza huyo baada ya kupata mbadala wake huku mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.

Aubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 akiichezea Dortmund tangu 2013, ikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.

Lakini alipigwa marufuku na klabu hiyo ya Ujerumani katika mechi yao dhidi ya Wolfsburg tarehe 14 Januari kwa kukosa mkutano wa timu.

Mshambuliaji huyo pia aliwachwa nje kwa mechi yao dhidi ya Hertha Berlin kwa sababu maafisa wa klabu hiyo walihisi hakuwa na malengo lakini alicheza dakika 90 katika mechi ya Jumapili dhidi ya Freiburg.

LEAVE A REPLY