Klabu ya Arsenal ya Uingereza wamekubaliana na Bolton Wanderers kwaajili ya msajili beki wa timu hiyo, Rob Holding kwa ada ya uamisho wa paundi milioni 2.

Beki huyo mwnye umri wa miaka 20 ni zao la timu ya vijana ya Bolton na alikuwa miongoni mwa kikosi cha Uingereza chini ya miaka 21 kilichoshinda taji la mashindano ya Toulon kipindi cha majira ya joto.

Holding pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Bolton Wanderers msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *