Mwanamuziki wa Marekani, Ariana Grande amewatembelea baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na bomu jijini Manchester dakika chache baada ya kumalizika kwa shoo yake.

Uamuzi huo unakuja baada ya wiki moja kupita msanii huyo alipofanya shoo jijini Manchester kwenye ukumbi wa Manchester Arena, wenye uwezo wa kuchukua watu 21,000 na kutokea mlipuko wa bomu ulioua watu 22 na majeruhi 119.

Ariana Grande alianza kutembelea katika Hospitali ya ‘Royal Manchester Children hospital’ ambapo kulikuwa na baadhi ya watoto waliolazwa kutokana na kuathirika na mlipuko huo.

“Kabla ya kuanza kwa shoo yangu leo (jana), nimeanza kwa kuwatembelea baadhi ya watoto waliojeruhiwa na mlipuko wa bomu, furaha yangu ni kuwaona wakiendelea vizuri,” alisema Ariana.

Siku ya Jumapili msanii huyo alikuwa na ratiba ya kufanya shoo ya kuwafuta machozi ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao, huku mastaa kibao akiwamo Justin Beiber, Pharrell Williams na wengine wengi wakiungana naye kutumbuiza katika shoo hiyo iliyopewa jina la ‘All Star Benefit Concert’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *