Michezo mitano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi imecheza kwa ukanda wa Marekani ya Kusini.

Brazil wakicheza katika dimba la Belo Horizonte, wamewachapa Argentina kwa mabao 3-0, mabao ya brazili yakifungwa na Philipe Couthino, Neymer, na Paulinho.

Venezuela wakicheza nyumbani nao wameibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwachapa bolivia kwa mabao 5-0.

Paraguay wamekubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-1 na Peru,Uruguay wakashinda kwa mabao 2 – 1 dhidi ya Ecuador

Colombia wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoshana nguvu na Chile kwa sare ya bila kufungana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *