Apple inatarajiwa kuzindua simu mpya ya iPhone 7 wengi wakitarajia kuona ikiwa simu hiyo mpya itaendelea kutumia kifaa ya kusikizia sauti yaani headphone jack.

Uzinduzi huo unafanyika siku chache baada ya mshindani mkubwa wa kampuni hiyo Samsung kulazimika kusitisha uuzaji wa simu yake ya kisasa zaidi ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri.

iPhone 2

Wachanganuzi wa masuala ya teknolojia wanaendelea kujadiliana kuhusu sifa na vifaa vipya ambavyo huenda vikazinduliwa kwenye simu hiyo mpya.

Wengi wanatarajia Apple itupilie mbali tundu la kuwekwa headphone jack na badala yake kuwe na tundu moja pekee.

Baadhi ya ammbo mapya yaliyozinduliwa karibuni zaidi kwenye iPhone yamekosa kuvutia watu sana.

iPhone3

Na wengi wanatarajia hilo lifanyike baada ya uzinduzi Jumatano mjini San Francisco, California.

Uwezo wa kamera hata hivyo unatarajiwa kuimarishwa zaidi. Huenda simu hizo zikawa na lens mbili za kamera ambazo zitamuwezesha mtu kupiga picha za ubora wa hali ya juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *