Kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuwanoa mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya England.

Conte katika msimu wake wa kwanza ameisadia Chelsea kutwaa ubingwa wa England kwa kushinda michezo 30,na kucheza fainali ya michuano ya kombe la Fa licha ya kufungwa na Arsenal katika fainali.

Baada ya kusaini mkataba huo mpya Conte alisema ” nina furaha sana kwa kusaini mkataba huu mpya,”

Nae mkurugenzi wa klabu hiyo Marina Granovskaia, aliongeza kwa kusema “mafanikio makubwa waliyopata, pamoja na uhodari wa kocha huyo ndio kimewapa imani ya kumuongezea Conte mkataba mpya”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *