Pambano la ndondi kati ya bondia Anthony Joshua wa Uingereza na Wladimir Klitshchko wa Ukraine linatarajiwa kufanyika Aprili 29 katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza mwaka huu.

Mambondia hao wamefanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Madison Square Garden mjini New York nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza tarehe hiyo.

Pambano hilo kwa ajili ya kuwania mataji ya IBF, IBO na WBA uzito wa juu ambapo kila mmoja amejitamba kunyakua mataji hayo.

Pambano hilo ni la kwanza kuwakutanisha mabondia hao wa uzito wa juu dunia ambao wametambiana sana kuelekea pigano hilo litakalofanyika katika uwanja wa taifa ya Uingereza, Wembeley.

Klitshchko ameshawahi kupambana na waingereza kama vile Tyson Furry ambapo Klitshcko alipigwa kwenye pambano hilo pia alishawahi kupambana na bondia David Haye ambapo Klitschko alishinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *