Pambano la ndondi linalosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko linalotarajiwa kufanyika kwenye uwanja Wembley nchini Uingereza linatarajiwa kuvunja rekodi ya watazamaji.

Pambano hilo la uzito wa juu linatarajia kufanyika terehe 29 mwezi Aprili.

Rekodi inayotarajiwa kuvunjwa kwenye pambano hilo ni idadi ya watazamaji ambao wanatarajia kufikia 90,000.

Meya wa jiji la London, Sadiq Khan anadaiwa kufanya jitihada kuongeza maafisa kutoka chama cha reli na chama cha wasafiri wa jiji hilo na uwanja wa Wembley kuhakikisha kuwa uwezo wa uwanja huo kuongeza nafasi 10,000 zaidi unafanikiwa kwaajili ya pambano hilo.

Pambano hilo litakuwa la kuwania ubingwa wa mikanda ya IBF unaoshikiliwwa na Joshua pamoja na mikanda ya WBA ‘super’ na IBO iliyotemwa na Tyson Furry.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *