Bondia wa Uingereza, Anthony Joshua amesema kuwa anataka kuwa kama Cristiano Ronaldo kwenye upande wa ndondi.

Bingwa huyo wa uzito wa juu wa IBF, Joshua amekusudia kuwa bora kwenye uapnde wa ngumi gkama alivyo nyota wa Real Madrid na Ureno, Ronaldo.

Joshua amesema anaweza kuanza umaarufu wake kwa kumpiga mpinzani wake, Wladimir Klitschko ifikapo Aprili 29 mwakani.

Joshua mwenye umri wa miaka 27 atakumbana na bingwa wa zamani katika pambano hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki 90,000 kwenye Uwanja wa Wembley.

Joshua, ambaye ana rekodi ya kushinda mapambano yake yote 18 kwa ‘KO’ amesema kuwa anampenda Cristiano Ronaldo kwa jinsi alivyoweza kukaa katika kiwango cha juu kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *