Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mnamo June 26, 2016 , Rais Magufuli alitengua Uteuzi wa Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Anne Kilango Malecela siku chache tu baada ya kuapishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Bi. Zainab R. Telack.

Kilichomng’oa mama huyo katika nafasi yake ni suala la wafanyakazi hewa ambapo tamko alilotoa kwamba mkoa wake haukuwa tena na wafanyakazi hewa wakati walikuwa bado wapo lilimgharimu nafasi hiyo na “kumrudisha nyumbani”.

Bi. Anne Kilango Malecela ni mke wa Mzee Malecela ambaye ni mmoja wa wakongwe wa kisiasa wachache waliobaki na ambao walishiriki harakati za kupigania uhuru wa nchi hii bega kwa bega na hayati Mwalimu Nyerere, aliwahi kushika nyadhifa nyingi za kisiasa nchini zikiwemo, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Uchukuzi, Balozi Uingereza, na kadhalika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *