Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amepinga uamuzi wa chama cha ACT-Wazalendo kumvua uenyekiti wa chama hicho.

Anna Mghwira amesema hayo jana alipofika ofisini kwake kwa mara ya kwanza na kupokewa watumishi wa ofisi yake.

 Amesema kuwa Baraza la Uongozi halina mamlaka ya kumuondoa kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama.

Alisema kuwa waliomvua madaraka ni Baraza Kuu la Chama lakini mamlaka ya kumpumzisha mwenyekiti yamekasimiwa kwa Mkutano Mkuu wa Chama kwa mujibu wa katiba ya ACT Wazalendo.

Akizungumzia uamuzi huo alisema hata Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa CCM, lakini bado anatumikia nafasi yake ya urais.

Anna Mghwira amekuwa kiongozi wa kwanza wa chama cha upinzani ngazi ya juu kuteuliwa serikalini.

Anna Mghwira aliyeteuliwa kushika nafasi iliyoachwa wazi na Meck Sadick alisema uamuzi huo kwa upande mwingine umempunguzia majukumu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *