Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa mkoa huyo mpya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck Sadick ambaye alijiuzulu mwezi uliopita.

Mkuu wa mkoa mpya wa Kilimanjaro, Anna Mghirwa akila kiapo mbele ya Rais Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa mpya wa Kilimanjaro, Anna Mghirwa akila kiapo mbele ya Rais Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

Sherehe za kuapishwa kwa mkuu wa mkoa huyo zimefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo alikula kiapo cha uongozi huo.

Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi.

Uteuzi wa kiongozi huyo umefanywa wiki iliyopita ambapo umezua gumzo kutokana na kuwa upande wa upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *