Mastaa wa Hollywood, Angelina Jolie na Brad Pitt wanatarajia kutalikiana hivi karibuni baada ya Jolie kufungua kesi ya kudai talaka mahakamani.

Wakili wa Angelina Jolie, Robert Offer, amesema kwenye ombi hilo mteja wake hahitaji msaada wa Pitt kwaajili ya malezi ya watoto wao sita.

Tovuti ya habari za wasanii mashuhuri ya TMZ imesema Jolie aliwasilisha nyaraka za kuomba talaka kortini Jumatatu, akitaja sababu ya kuachana kwao kuwa ni ‘tofauti zisizoweza kusuluhishwa’.

Kwenye maelezo yake, Jolie ameomba mahakama imruhusu kuishi na watoto wao huku akiiomba mahakama hiyo impe Pitt ruhusa ya kuwatembelea watoto hao.

Wawili hao walianza uhusiano wa kimapenzi wakati walipokuwa wakitengeneza filamu ya ‘Mr & Mrs Smith’ mwaka 2004, wakati huo Brad Pitt akiwa kwenye ndoa na staa mwengine wa filamu Jeniffer Aniston.

Wawili hao walikuja kufunga ndoa Agosti 2014 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka 10.

Kwenye maisha yao ya ndoa wamejaaliwa kupata watoto mapacha Knox na Vivienne huku wakiasili watoto wengine wanne Maddox, Pax, Zahara na Shiloh.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *