Muigizaji nyota wa Marekani, Angelina Jolie amesema kuwa Brad Pitt ataendelea kuwa mume wake daima licha ya kuachana.

Jolie amefunguka hayo kwa mara ya kwanza tangu kusambaa kwa taarifa za kuachana na mume wake huyo ambaye pia ni muigizaji nyota wa Marekani ambapo wameachana mwishini mwa mwaka jana.

Muigizaji huyo amesema kuwa, alikuwa katika wakati mgumu kuelezea kilichotokea kati yake ya mume wake, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na maisha yanaendelea kama kawaida.

Mkali huyo amesema kuwa “Nilikuwa nashindwa kuelezea kilichotokea, lakini kwa sasa naweza kusema kuwa kila kitu kipo sawa, Brad Pitt ataendelea kuwa baba wa familia yangu.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa “Najua hali niliyoipitia mimi watu wengi wamepitia, najua sikuguswa peke yangu, kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza ni watoto wangu, lakini nina furaha kubwa kumaliza tofauti zetu,”.

Angelina Jolie aliamua kuomba talaka kwa mume wake huyo kutokana na taarifa kuwa Brad Pitt yupo kwenye mahusiano na mwanamke mwingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *