Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki amekanusha tetesi kuwa serikali itaanza kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao.

Waziri huyo amelazimika kutumia akaunti  yake ya Twitter kukanusha taarifa hizo alizoziita za uongo.

Kairuki ameandika “Kuna taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao, Ipuuzieni,”.

Pia ameongeza kwa kuandika “Si dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya watumishi wa umma hususani matumizi ya mishahara yao. Ipuuzieni uzushi huo”.

Angela Kairuki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *