Aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwae Anerlisa Muigai amefichua sababu ya kuachana na mume wake kisa alikuwa mchafu jikoni.

Anerlisa ambaye hakubahatika kupata mtoto na Ben Pol ambaye pia ni mfanyabishara mkubwa ameibuka na jipya akisema kuwa, aliwahi kumuacha mwanaume kisa alikuwa mchafu jikoni.

Anerlisa amefunguka hayo wakati akijibu moja ya video iliyopostiwa kwenye Instagram ikimuonesha mwanaume ambaye hajasafisha jiko.

Anerlisa alijibu video hiyo kwa emoji ya kucheka akisema aliwahi kumuacha mwanaume ambaye alikuwa na tabia ya uchafu kama huo.

Jibu hilo la Anerlisa limeibua maswali na sintofahamu kwamba huwenda anayezungumziwa ni Ben Pol kwa sababu ndiye EX-Husband wake anayefahamika zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *