Bingwa wa Olimpiki wa mchezo wa tennis, Andy Murray ameshindwa kudhibitisha ubora wake mbele ya Marin Cilic baada ya kufungwa kwa seti 6-4 7-5 katika fainali iliyofanyika mjini Cincinnati.

Hii ni wiki moja baada ya kuweka rekodi kwenye michuano ya Olimpiki iliyofanyika Mjini Rio nchini Brazil.

Bingwa huyo anaeshikilia nafasi ya pili duniani, Murray alikuwa anajaribu kulinda nafasi katika mashindano makubwa ya Cincinnati, baada ya kushinda mwaka 2008 na 2011.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Cilic mwaka 2016 na wa tatu tangu michuano ya wazi ya Marekani mwaka 2014.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *