Mchezaji tenisi wa Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kumfunga Novak Djokovic na kunyakua tuzo ya kwanza ya fainali za Dunia za ATP 2016 akiwa kama mchezaji namba moja duniani.

Akiwa katika kiwango cha juu Mwishoni mwa mwaka, Murray ameshinda fainali hizo kwa 6-3 6-4 katika uwanja wa O2 arena mjini London

Akiongeza kuwa ni nafasi ya kipekee sana kushindana na Novak katika mashindano kama haya.

Murray mwenye umri wa miaka 29 amekuwa mchezaji bora katika mashindano 24.

Mashindano hayo pia yalimalizika kwa ushindi wa miaka minne wa Djokovic katika kinyan’ganyiro na Msebia huyo huku akimkaribia Roger Federer’s.

Murray aliyeshinda vikombe 34 kwa mara kumi ameongeza ” kabla ya hapa tumekuwa tukichuana katika fainali mbalimbali na katika Olimpiki lakini ninayo furaha kubwa kuwa mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *