West Ham United imekamilisha usajili wa mchezaji, Andre Ayew kutoka Swansea City kwa ada ya paundi milioni 20 na kuweka rekodi ya klabu hiyo akiwa mchezaji ndiye aliyenunuliwa kwa ela nyingi.

Mshambuliaji huyo raia wa Ghana amesaini mkataba wa miaka mitatu na wagonga nyundo hao wa London ambapo atakaa ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2019.

jordan

Andre Ayew amecheza msimu mmoja ndani ya klabu ya Swansea City akitokea timu ya Marseille ya nchini Ufaransa mwaka jana.

Mshamuliaji huyo baada ya kusainiwa na klabu hiyo alisema kwamba anajisikia furaha kujiunga na West Ham United kwani ni timu bora na amehaidi kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *