Bayern Munich itatoa tangazo kuhusu hatma ya kocha Carlo Ancelotti baadaye leo baada ya kupoteza mechi dhidi ya Pars St. German.

Bodi ya timu hiyo ilikutana baada ya kichapo hicho kutoka kwa matajiri wa Ufaransa kwemye mechi za klabu bingwa Ulaya.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alichukua nafasi ya Pep Guardiola mwanzo wa msimu wa 2016-17.

Ancelotti aliisaidia Bayern kushinda kombe la Bundesliga , lakini klabu hiyo ikatolewa kwenye ligi ya mabingwa msimu uliopita.

Walishindwa kufika katika fainali ya DFB baada ya kushindwa 3-2 na Borussia Dortmund.

Ancelotti ameshinda kombe la vilabu bingwa mara tatu mbali na mataji ya ligi nchini Itali, Uhispania, Uingereza na Ujerumani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *