Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa kimaeneo yakitarajiwa kutolewa leo nchini Afrika Kusini huku ikibainika wazi kuwa chama cha ANC kimeibuka na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi kuwahi kushuhudiwa.

Chama cha Democratic Alliance kimeibuka na ushindi mkubwa na muhimu katika baraza la manispaa ya Nelson Mandela Bay.

Chama cha ANC kinajitahidi kuchukua udhibiti wa miji ya pretoria na Johannesburg.

Hata hivyo, ANC inasalia kuwa chama maarufu katika siasa za Afrika Kusini, kwa kuzoa aslimia 54 ya kura hizo.

Chama cha Democratic Alliance kimekuwa kikiungwa mkono na wazungu pamoja na chotara japo wapiga kura weusi wameanza kukiunga mkono, kwa kukatishwa tamaa na mwendo wa kobe wa uimarishaji wa uchumi wa chama tawala cha ANC, na sakata nyingi zinazomkabili rais wa sasa Jacob Zuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *