Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Amissi Tambwe yupo fiti kuwavaa Medeama katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Tambwe ambaye alikosekana katika mechi dhidi ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Congo kutokana na kuwa majeruhi ambapo katika mechi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Yanga ilifungwa 1-0.

Mshambuliaji huyo alianza mazoezi mepesi ya binafsi katika uwanja wa Boko veterani jijini Dar es Salaam ambapo timu yake pia inafanya mazoezi katika uwanja huo.

Yanga hapo kesho italazimika kushinda mechi hiyo ili kuwa na nafasi ya kuweza kusonga mbele baada ya kupoteza mechi mbili za nyuma ambapo mechi ya kwanza ilifungwa dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na ya pili dhidi ya TP Mazembe.

Tambwe: Akishangilia moja ya goli lake katika mechi ya ligi kuu

Tambwe: Akishangilia moja ya goli lake alilofunga katika mezi ya ligi kuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *