Video queen wa Bongo, Amber Lulu amesema kuwa familia yake haifuatilii mitandao ndiyo mana anafanya anavyotaka kwenye mitandao hiyo ya kijamii pamoja na kupiga picha za utupu.

Amber Lulu amesema kuwa familia yake siyo ya mitandaoni kwahiyo kwake ni sawa kuweka picha za utupu kupitia akaunti zake tofuati za mitandano ya kijamii kama vile Instagram na Facebook.

Video Queen huyo amesema hayo leo wakati akifanya mahojiano na kituo maarufu cha Radio nchini.

Amesema kuwa  “Familia yangu hawafatilii mitandao ya kijamii na hata wakiona picha zangu kwa sasa wanaelewa nini nafanya.

Ameongeza kwa kusema kuwa ‘Siyo kila kitu tunachoposti kwenye mitandao ya kijamii ndivyo maisha yetu tunayoishi”.

Kabla ya kuingia katika muziki na kutangaza kuachana na u-video vixen, Amber Lulu alishatokea kwenye video kama Inde ya Harmonize na Dully Sykes.

Amber Lulu amejizolea umaarufu nchini kupitia mitandao ya kijamii kutokana na kuweka picha za utupu (half naked) kwenye mitandao hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *