Video vixen anayefanya vizuri kwasasa nchini, Amber Lulu amekanusha tetesi kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki, Country Boy ambaye wamefanya nyimbo ya pamoja.

Amber Lulu amesema kuwa anamkubalia sana Country Boy, huku akikiri kuwa mahusiano ya Young Dee licha ya kupiga chenga kuwa mahusiano yake na Country Boy ni ya kikazi pekee na hayatahusu mapenzi.

country-boy

Video vixen huyo ameleza kinachomvutia zaidi kwa Country Boy ikilinganishwa na wasanii wengine wa kiume katika game ya Bongo Fleva.

Akiwa ameingia rasmi kwenye game ya bongo fleva kama msanii wa kuimba, amesema mastaa wengi wa kiume ambao amekuwa akifanya nao kazi, wamekuwa wakishindwa kujizuia na kutamani mapenzi zaidi ya kazi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *