Mwanamuziki wa Muziki wa Dansi nchini, Ally Choki amekanusha tetesi zilizogaa kuwa msanii huyo ameihama bendi yake ya Twanga Pepeta ambapo amethibitsha siyo kweli.

Ali Chocky amesema kuwa madai hayo yaliyokuwa yakienea chini kwa chini kuwa siyo ya kweli kwasababu yeye bado ni mwanamuziki wa Twanga Pepeta mpaka mkataba wake utakapomalizika.

Chocky amesema kuwa wanaoeneza madai hayo wana sababu zao ila mashabiki wake wajue tu kuwa yeye yuko Twanga hadi mwaka 2018 kutokana na mkataba wake.

Choki amesema “Mkataba wangu hapa Twanga unaisha mwaka 2018, sasa hao wanaosema nahama Twanga sijui wanatoa wapi hizo habari,”.

Ally Choki ni mwanamuziki mongwe wa muziki wa Dance nchini kutokana na kuanza muziki toka miaka ya 2000 hadi sasa anaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo ya muziki wa Dance japokuwa muziki huyo kwasasa kushuka kiwango.

                                                                                         

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *