Baada ya kuteuliwa na rais kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage amesema atafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na kwa kufuata sheria, kanuni na Katiba ya nchi.

Jaji Kaijage ametoa msimamo huo baada kuulizwa namna gani ataitumikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imekuwa inalalamikiwa na baadhi ya vyama vya siasa kuwa haiko huru kutokana na watendaji wake kuteuliwa na Rais.

Uteuzi wa Jaji Kaijage ambao umefanywa na Rais John Magufuli, ulitangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

Jaji Kaijage amechukua nafasi ya Jaji mstaafu Damian Lubuva ambaye muda wake wa kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo umemalizika hivi karibuni.

Mwenyekiti huyo mpya ataiongoza NEC kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *