Muigizaji wa Bongo movie, Chuchu Hansy amezungumzia sababu ya ujauzito wake na kusema kuwa hajataka kuweka hadharani kwani ni kitu binafsi.

 

Chuchu Hansy amesema taarifa za yeye kuwa na ujauzito ameamua kufanya siri kwani anaona si vyema kuzungumzia vitu binafsi hadharani hususani kwenye mitandao na kwamba muda muafaka ukifika kila mmoja atajua ukweli.

 

Kauli hiyo ya Chuchu inakuja kufuatia maneno ya watu kuwa muigizaji huyo anaficha ujauzito uhenda kuna sababu inayofanya hivyo lakini mwenyewe amefunguka na kusema kuwa ni maisha binafsi.

 

Muigizaji huyo yupo kwenye mahusiano wa muigizaji mwenzake Vicente Kigosi maarufu kama Ray na ujauzito huo unahisi ukawa wa Ray kutokana na mahusiano yao.

 

Chuchu Hansy amekuwa gumzo mtandaoni kwa kuficha taarifa za ujauzito wake, tofauti na wasanii wengi wa kike wanavyofanya siku hizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *