Raia wa Uingereza, Michael Sandfgord amehukumiwa kifungo cha miezi 12 kwenda jela kufuatia jaribio lake la kutakata kumuua rais mteule wa Marekani, Donald Trump.

Michael Sandfgord mwenye umri wa miaka 20 alikiri makosa hayo ya kumiliki bunduki na kuvurua mkutano.

Analaumiwa kwa kujaribu kunyakua bunduki kutoka kwa polisis wakati wa mkutano wa hadhara huko Las Vegas ili kumfyatulia risasi mgombea urais.

Mahakama imesema kuwa huenda akaachiliwa baada ya miezi minne ambapo atasafirishwa hadi nchini Uingereza

Baada ya Sandford kukamatwa aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kumpiga risasi Donald Trump.

Mamake amesema kuwa alikuwa amepoteza mawasiliano na mwanawe, ambaye aliondoka nyumbani kutembea kote marekani mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *