Aliyemuuwa mpenzi wake na kumchoma moto akamatwa Afrika Kusini

0
251

Kijana aliyemuuwa mpenzi wake na kumchoma moto Afrika amekamatwa na jeshi la Polisi nchini humo.

Polisi wa nchini Afrika ya kusini wamethibitisha kumshikilia kijana wa miaka 27  na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mpenzi wake Karabo Mokoena mwenye umri wa miaka 22 aliyeripotiwa kupotea wiki mbili zilizopita.

Mwili wa binti huyo ulikuwa ukiwa umechomwa na ilikuwa vigumu kuutambua.

Wanawake wengi wa nchini humo kupitia mitandao ya kijamii walionyesha kukasirishwa na kitendo hicho na kulaumu vitendo vya uonevu dhidi ya wanawake.

Nchi ya Afrika Kusini imeripotiwa kuwa na matukio mengi ya udhalilishaji na vitendo vya uonevu kwa wanawake ikiwamo ubakaji kwa muda mrefu sasa.

LEAVE A REPLY