Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imetoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Television cha chanel Ten, Daud Mwangosi.

Mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 mshtakiwa wa mauaji hayo, askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’, Pacificius Simon.

Hukumu hiyo imekuja baada ya juzi mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 mwaka 2012 kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi  mkoani Iringa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *