Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani, Park Geun-hye ameshtakiwa kuhusiana na kashfa ya rushwa iliyopelekea kung’atuliwa kwake uongozini.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa mashtaka yanayomkabili ni kupokea hongo, utumizi mbaya wa mamlaka, na kudukua siri za serikali.

Park, 65, ambaye yupo kizuizini, ameshtakiwa kwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kutoza fedha kampuni kadha kuu ili wapendelewe kisiasa.

Alipoteza kinga yake na kutolewa mamlakani baada ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha uamuzi ya bunge kumng’atua uongozini.

Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake wa kirais ili kuweka shinikizo kwa kampuni kutoa mamilioni ya madola katika michango kwa mashirika yasiyo ya serikali ambayo anayashikilia.

Bi Park anadaiwa kuhusika binafsi katika masuala hayo, na kumpa Bi Choi ruhusa isiyokubalika kupata nyaraka rasmi.

Kaimu Kiongozi wake Lee Jae-yong na Bi Choi wamewekwa pamoja kizuizini huku Bi park akingojea kesi dhidi yake ianze.

Mwenyekiti wa kampuni ya Lotte Shin Dong-bin alishtakiwa kutoa rushwa Jumatatu, lakini viongozi wa mashtaka hawakumweka kizuizini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *