Aliyekuwa rais wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amekamatwa na polisi kufuatia uchunguzi wa ulanguzi wa fedha.

Baadhi ya watu wengine pia walikamatwa baada ya polisi kuvamia ofisi tisa na nyumba kaskazini mashariki mwa Catalonia nchini Uhispania.

Hatua hiyo nio miongoni mwa haki za mauzo zinazoshirikishwa na Brazil kulingana na duru za maafisa wa polisi.

Rosell alikuwa rais wa Barcelona kutoka mwaka 2010 hadi 2014, wakati alipojiuzulu kufuatia uamuzi wa mahakama ya Uhispania kuchunguza usajili wa mchezaji wa Bacelona, Neymar mwaka 2013.

Mnamo mwezi Juni 2016, Barcelona ililipa faini ya Euro milioni 5.5 kufuatia uhamisho wa mchezaji huyo kutoka klabu ya Santos nchini Brazil.

Klabu hiyo ilishutumiwa kwa kukwepa kulipa kodi jambo ambalo klabu hiyo inalipinga vikali swali hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *