Mwanariadha wa Marekani, David Torrence amekutwa amefariki katika bwawa la kuogelea katika jimbo la Arizona nchini Marekani.

Torrence mwenye umri wa miaka 31 alishinda fedha katika mbio za ubingwa wa dunia za kupokezana vijiti mwaka 2014 na alimaliza wa pili pia katika mbio za bara la Amerika mwaka 2015.

Alibadilisha uraia kutoka Marekani hadi Peru na akawakilisha taifa hilo lake jipya katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016.

Taarifa ya kifo chake ilisema kuwa “Wachunguzi wa jinai wamebaini kwamba hakuna dalili zozote dhahiri kwamba huenda aliuawa,”.

David Torrence alimaliza wa 13 mbio za 5,000m upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016 ambapo Mo Farah alishinda dhahabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *