Aliyekuwa meneja wa kundi la N.W.A, Jerry Heller amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari siku ya Ijumaa na amefariki akiwa na miaka 75.

Baada ya ajili hiyo alikimbizwa hospitalini baada ya majeraha makubwa kutokana na kugongana na gari aina ya mini-van lakini hakuweza kufanikiwa na kufariki njiani akiwahishwa hospitali.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ni wazi kuwa kifo chake kilitokana na matatizo ya afya, ajali, au yote mawili.

Meneja pia aliwahi kufanya kazi na Elton John, Pink Floyd, The Who, na wengineo katika miaka ya 60 na 70.

N.W.A: Kundi lililokuwa linaongozwa na Jerry Heller ambaye kwasasa ni marehemu.
N.W.A: Kundi lililokuwa linaongozwa na Jerry Heller ambaye kwasasa ni marehemu.

Baada ya hapo Jerry alianza kulisimimamia kundi la N.W.A kwa miaka minne katika miaka ya 1980, toka siku lilipozinduliwa.

Kundi la N.W.A lilikufa baada ya kuibuka migogoro ya mirabaha kati ya meneja huyo wasanii wawili Dr. Dre na Ice Cube kuliibuka tofauti ya hadharani na kusababisha kusambaratika kwa kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *