Tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote ameonyesha nia ya kuwekeza kwenye muziki.

Mwaka jana mfanyabiashara huyu alionekana na P Square na kutengeneza vichwa vya habari kuhusu colabo hio.

Aliko Dangote hivi karibuni alikuwa na staa wa muziki kutoka Mavin Records Korede Bello ikiwa ni matayarisha kuelekea kutoka kwa album ya msanii huyu Belloved mnamo March 11 mwaka huu.

Tunasubiri kusikia kiasi gani cha pesa Aliko atawekeza kwenye muziki wa Korede Bello.

Tajiri huyo ameamua kuwekeza kwenye muziki baada ya kuwekeza kwenye mambo ya viwanda lakini sasa ameamua kukita nguvu kwenye muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *