Staa wa Bongo fleva, AliKiba amefunguka na kusema kwamba watanzania walizidiwa na wasanii kutoka nchi nyingine kwenye tuzo za MTV Mama Awards zilizofanyika wiki ilyopita jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mkali huyo amesema watanzania walijitahidi lakini walizidiwa na wasanii wa nje ndiyo maana wakashindwa kutamba.

Vile vile aliongeza kwa kusema kuwa kwasasa muziki wa kitanzania umekuwa na unazidi kutanuka kwa hiyo kushindwa kutamba kwenye tuzo za MTV si sababu ya kukata tamaa inabidi tusonge mbele.

Alikiba alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wanawania tuzo hizo kwenye kipengele cha ‘Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae alioshirikiana na Sauti Sol kutoka Kenya.

Kwenye tuzo hizo Alikiba pia alipata fursa ya kutumbuiza kwenye siku ya utoaji tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Ticketpro Dome jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini katika.

Kwa upande mwingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa kolabo yake mpya ya kimataifa.

Alikiba kwasasa anatamba na wimbo wake Aje ambao unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na TV nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *