Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Alikiba amesema kuwa tayari ameshajisajili kushiriki kwenye tuzo za East Africa Televison ‘EATV Awards’ zilizoandaliwa na kituo cha TV cha EATV.

Alikiba amesema ni jambo jema lililofanywa na EATV kuweza kutambua thamani ya wasanii na kazi zao za sanaa kwa kuleta tuzo hizo.

Kiba aliendelea kusema kuwa “Mimi tayari nimeshajisajili kushiriki tuzo hizo, mimi naona EATV wameonesha jinsi gani wanajali uwepo wa wasanii ambao wanastahili kupata tuzo, ingawa natambua kutakuwa na ushindani mkubwa kutoka katika nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi lakini niseme tu naamini sisi Tanzania tupo vizuri zaidi si kama naipendelea kwa kuwa ni nchi yangu hapana lakini watu wapo ‘Serious’ na kazi na kila mtu yupo ‘serious’ na kitu anachofanya hivyo naamini ushindani ni mkubwa sana”.

Tuzo hizo za EATV zinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ifikapo mwezi Disemba

Kwa upande mwingine mwanamuziki huyo anatarajia kuperfom kwenye utoaji wa tuzo za MTV MAMA zitakazofayika katika jiji la Journesburg nchini Afrika kusini Oktoba 22 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *