Mkali wa ‘Aje’ Alikiba na kundi la Sauti Sol jana walipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini kufuatia utoaji wa Tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika leo.

Tuzo za MTV MAMA huwa na shughuli nyingi za awali siku moja kabla ya usiku wenyewe wa utoaji ambao kwa mwaka huu utolewa leo.

Kwenye mahujiano hayo  Alikiba na Sauti Sol wanaowania pamoja tuzo  walizungumzia kuhusiana na ushirikiano wao na mambo mengine.

Kwenye tuzo hizo kubwa barani Afrika Sauti Sol wanagombania tuzo ya nyimbo bora ya kushirikiana ambayo nyimbo iliyoingia ni Unconditionally Bae walioshirikiana na Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *