Ni jambo ambalo unaweza usiamini kuwa limemtokea super star wa Tanzania Ali Kiba. Kwa hadhi aliyonayo na nafasi yake kwenye muziki wa Bongo ni wazi kuwa Kiba ni mmoja wa mastaa ambao wanatafutwa sana na mastaa wa nchi nyingine kwaajili ya kufanya collabo, lakini IWEJE leo aje atendewe hili?

Kiba ameeleza ukweli wa sababu iliyopelekea staa wa Nigeria, MI kutoonekana kwenye video ya remix ya ngoma yao ya collabo ya AJE.

Ngoma hiyo ambayo original version imefanywa na Kiba mwenyewe, imeshindwa kuwa na sura ya MI kwenye video ya remix hiyo kwasababu ‘staa’ huyo ‘ANAJALI ZAIDI BIASHARA ZAKE’, hayo ndio maneno ya Kiba.

KING kama anavyofahamika kwa fans wake wengi, amedai kuwa menejiment yake ilijaribu bila mafanikio mara mbili kumtafuta MI na kumaktia tiketi za ndege ili aungane nao kwaajili ya kuandaa video hiyo lakini hakutokea.

Mwishowe ikambidi atengeneze video hiyo bila sura ya MI.

Kiba ni wa kwanza? NO, haya ni maneno aliyonukuliwa akiyatoa Rich Mavoko kuhusiana na ngoma yake KOKORO.

‘Kuna msanii alitakiwa akae kutoka Nigeria mishe zikawa nyingi hapa na pale, hivi imekuwa hivi, vile imekuwa hivi, tutafanya hivi, muda unaenda’.

Mavoko akaamua kumpa shavu Diamond Platnumz.

Je, baada ya hapo mastaa wanaoombwa collabo au wanaoshirikishwa wakishawatosa mastaa wa Bongo huomba radhi?

Mastaa wa Bongo WANAWANYENYEKEA sana mastaa wa nje?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *