Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Alikiba ametajwa kuwania  tuzo za mwaka huu za zijulikanazo kama ‘MTV Europe Music Awards’  (EMA) akiwa katika kipengele cha Best African Act.

AliKiba mekuwa mwanamuziki pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania kipengele hicho.

Kiba atachuana na wasanii wengine wakiwemo Wizkid na Olamide wa Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.

Mshindi katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond Platnumz.

Vile vile Alikiba yumo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za MTV MAMA ambapo nyimbo aliyeshirikishwa na Saut Soul kuwania tuzo ya nyimbo bora ya kushirikiana na pia atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotoa show katika tuzo hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *