Kilele cha tamasha la Fiesta kinatarajia kufikia tamati leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Jukwaa la tamasha hilo litashereheshwa na wasanii wa ndani na nje ya nchi watakaotoa burudani kwenye viwanja hivyo vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Wasanii wa nje watakaotoa shoo ni Jose Chameleon kutoka Uganda, Tekno na Yemi Alade kutoka Nigeria ambao watashirikiana na wasanii wa ndani kuwapa burudani wanadar es Salaam leo.

Wasanii wa ndani ni pamoja na Alikiba, Baraka The Prince, Barnaba, Bell 9, Billnas, Chege, Christian Bella, Darassa, Dogo Janja, Fid-Q, Hamadai, Jay Moe, Juma Nature, Jux, Lord Eyez, Man Fongo, Maua Sama, Mr Blue, Msami, Nandy, Raymond, Roma, Shilole, Sholo Mwamba, Snura, Stamina, Vanessa Mdee, Weusi na Young Dee.

Kiingilio kwenye tamasha hilo la Fiesta itakuwa shilingi elfu 20 kwa kila tiketi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *