Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ambaye kwasasa anatamba na wimbo wa ‘Seduce Me’ anatarajiwa kutoa burudani kwenye Tamasha la Fiesta Septemba 19 mwaka mkoani Arusha.

Alikiba atakuwa miongoni mwa kundi la wasanii wa muziki watakaoangusha burudani kwenye Tamsha hilo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Wanamuziki zaidi ya 17 akiwemo Kiba wameshasajiliwa kwa ajili ya kutoa burudani katika Tigo Fiesta ambayo itafanyika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mbali na Kiba wasanii wengine waliosainiwa kutoa burudani ni Christian Bella, Shilole, John Makini, Mr. Blue, Saida Karoli na wengine kibao.

Fiesta ni Tamasha linaloandaliwa na kampuni ya Clouds Media ambalo ufanyika kila mwaka katika mikoa tofauti hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *