Wanamuziki nyota wa Tanzania, AliKiba na Nandy ni miongoni mwa wasanii 18 wa muziki walioteuliwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) zinazotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwa huu.

Wengine walioteuliwa ni pamoja Bebe Cool wa Uganda , Yemi Alade, AKA,

Runtown, Nasty C, Eddy Kenzo, Locko, Anselmo Ralph, Jah Prayzah, Busiswa, Amanda Black.

Orodha ya walioteuliwa ilitangazwa mwezi Agosti katika hoteli ya Renaissance mjini Lagos, Nigeria.

Orodha ya walioteuliwa ina makundi 33, ikiwemo 10 ya kieneo mbali na mengine 23 huku nyota wa Coke studio wakijizolea nafasi 25.

Katika tuzo nyengine ya Afrima ya baadaye nyota wengine wa Coke studio wameteuliwa katika kundi la kibara.

Wao ni Kiff No Beat (Ivory Coast) Mafikizolo na Mi Casa kutoka Afrika Kusini katika kundi bora la muziki Afrika.

Kwa msanii bora zaidi barani Afrika walioteuliwa ni Anselmo Ralph (Angola) na Alikiba (Tanzania).

Wimbo wa Aje ulioimbwa na Alikiba akishirikiana na MI pia umeteuliwa katika kepengele cha muziki bora uliofanywa kwa ushirikiano pamoja na Jah Prayzah’s Watora Mari akishirikiana na Diamond na Supporter.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *